UANZISHAJI NA UENDESHAJI WA KITUO CHA ELIMU

Uanzishaji na uendeshaji wa kituo cha elimu na mafunzo ya Ufundi katika kijiji cha Ilagala Shughuli hii ilianza kwa kutumia nguvu/michango ya wanachama ambapo lengo kubwa lilikuwa kuwa na kituo/chuo cha mafunzo ya ufundi kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili waweze kujimudu kimaisha. Hoja hii ilitokana na ukweli kwamba wengi wa watoto wanaotoka katika familila maskini hawamalizi darasa la saba na hata wale wanaomaliza hawapati fursa ya kuendelea na elimu ya sekondari jambo ambalo linawafanya waonekane watumwa katika nchi yao. Shughuli zinazoendelea kufanyika ni pamoja na:- 1. Ujenzi wa majengo mawili ambapo moja linatumika kama la utawala na lingine kama stoo 2. Kuweka mfumo wa umeme wa jua kwenye jengo la utawala 3. Kununua samani kwa ajili ya ofisi na madarasa 4. Kununua vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia 5. Kujenga madarasa saba ambayo mpaka sasa yanatumika 6. Kuendesha masomo katika fani za useremara, ushonaji, ujenzi pamoja na uchomeleaji vyuma.