UBORESHAJI WA ELIMU KWA WILAYA

Uboreshaji wa elimu kwa wilaya za Kasulu, Uvinza na Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mradi huu unafadhiliwa na WEKEZA ukiwa na lengo la kutokomeza utumikishwaji wa watoto. Shughuli zilizotekelezwa katika mradi huu ni pamoja na:- Kujenga uwezo wa kamati na bodi za shule kupitia mafunzo mbalimbali juu ya majukumu yao Kuongeza uwazi na uwajibikaji miongoni mwa wananchi na wajumbe wa kamati na bodi za shule kupitia mikutano mbalimbali miongoni mwa pande zote zinazohusika Kuendesha mikutano ya pamoja kati ya kamati, bodi za shule pamoja na kamati zingine za maendeleo katika kijiji/Kata Kukarabati shule zenye hali mbaya kuliko zingine ndani ya jamii.