UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI KIJAMII (SAM)

fuatiliaji wa uwajibikaji Kijamii (Social Accountability Monitoring) Mradi huu unafadhiliwa na The foundation for civil society Tanzania. Lengo la mradi huu ni kuwajengea uwezo wanajamii wa halmashauri za Kigoma vijijini, Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Uvinza katika kufanya ufuatiliaji wa uwajibikaji kijamii kwa kuangalia mipango inayopangwa, ushirikishwaji wa wananchi katika kubuni, kutekeleza, wanaoshirikije kufuatilia na kupima ubora wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Shughuli zilizofanyika katika kipindi hiki ni:- Kuendesha mikutano na watendaji wa kila wilaya na wadau wengine wa maendeleo hasa wanajamii wenyewe ili kujadiliana juu ya Takwimu za miradi ya maendeleo zilizopatikana (data validation) Kuendesha mafunzo juu ya mbinu za kufanya ushawishi, utetezi na utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo katika sekta ya elimu kwenye wilaya tajwa hapo juu.