Administrative message

Kwa heshma kubwa ninawakaribisha wasomaji wetu kwenye tovuti yetu ya Umoja wa wawezeshaji KIOO. Shirika letu lilianzishwa mwaka 2001 na kusajiliwa rasmi Novemba 9, 2004. Dhima ya shirika letu ni ‘‘Kuwawezesha wananchi hasa wale walio kwenye makundi yaliyosahaurika ili wafahamu haki zao na kisha waweze kuchukua hatua sahihi zinazolenga- kushawishi na kutetea haki zao na hatimaye waweze kuishi maisha bora yanayoheshimu haki za binadamu kwa maendeleo endelevu”

Shughuli zilizotekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa ni:-

  • Uendeshaji wa shughuli za elimu katika mfumo usio rasmi (ACCESS CENTRE & REFLECT), Lengo kubwa lilikuwa kupunguza wimbi la watu wasiojua kusoma na kuandika katika kata za Ilagala na Sunuka kwa kutumia mbinu ya REFLECT na ACCESS
  • Uhamasishaji wa jamii katika kujikinga na magonjwa ya zinaa ikiwamo UKIMWI kwa kutumia mbinu ya KIVUKO na baadaye STAR. Hizi ni mbinu ambazo huwaleta watu wa rika, elimu na uwezo (Social status) tofauti pamoja ili kujadiliana namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili kama jamii.
  • Uimarishaji wa utawala bora vijijini. Lengo kuu la mradi likiwa kuwajengea uwezo wanajamii waishio vijijini juu ya misingi ya utawala bora.
  • Ufuatiliaji wa raslimali za umma katika sekta ya elimu na Afya. Lengo kubwa la mradi huu lilikuwa kufuatilia matumizi ya raslimali za umma katika sekta ya Elimu na Afya katika wilaya za Kigoma, Kasulu na Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
  • Uimarishaji wa haki za kijamii katika kumiliki Ardhi. Lengo la kuhamasisha uelewa wa wanajamii waishio vijijini juu ya umhimu wa umiliki wa Ardhi kimila kama ilivyoelekezwa na sheria ya Ardhi Na 5 ya 1999.

Sisi kama shirika tunatamani kushirikiana na kila mmoja wenu kwa kadri ya uwezo wake, bado msaada wa kila mmoja tunauhitaji.

Ni matarajio yangu kuwa utafurahia kuisoma web site hii

Wako Katika ujenzi wa Taifa

Edward Bihaga Saimon

Mkurugenzi Mtendaji.